TUPIGIE SIMU! DAR IVF & FC
+255 684 633 777
Slide Dar IVF & Fertility Clinic #5

Kuhusu Dar IVF

Ninawakaribisha kwenye kliniki yetu mpya. Ninawaletea uzoefu wangu wa matibabu ya uzazi nilioupata kutoka Uingereza, Kuwait na Uganda. Huu uzoefu ni wa asili na ulitokana na msukumo kutoka kwa mama yangu mzazi Mganda, ambaye alikuwa mkunga wa jadi. Nilikuwa nasaidiana naye katika kutoa huduma ya uzazi kwa kina mama aliyokuwa akiifanyia nyumabani kwetu Masaka.

Naamini kwa msaada wa Mungu na wa wafanyakazi wetu wa kliniki ya Dar ambao wamebobea na kujizatiti katika kazi yao, itasaidia wanandoa wengi kupata mtoto baada ya kuwa wamekuwa wakijaribu kuwa na familia kwa miaka mingi bila ya mafanikio.

Naweza kusema kwamba hatuwezi kusaidia kila mtu ambaye ataingia milango ya kliniki yetu. Ila kwa muongozo mzuri na kujua tatizo, pamoja na motisha, subira na msaada wa kifedha,  naamini wanandoa wengi wana nafasi nzuri sana ya kupata mtoto.

Mtoto wa kwanza kuzaliwa kutumia teknologia ya IVF (upandikizaji) katika Dunia ni Louse Brown ambaye alizaliwa mwaka 1979 nchini Uingereza. Tangu wakati huo, watoto zaidi ya milioni 6 wamezaliwa duniani kote. Watoto waliozaliwa kwa njia hii (IVF) ni wakawaida kabisa na hawana tofauti na watoto ambao mimba zao zilitungwa kwa njia ya asili. Kipindi cha ujauzito, mimba ni sawa na mimba ya kawaida. Watoto ni wakawaida na hakuna tofauti na wale mimba zao zilitungwa kawaida. Matukio ya kasoro ya kuzaliwa ni sawa na watoto ambao mimba zao zilitungwa kwa njia ya asili. Kama jambo la kweli,  ukiuliza akina mama ambao wamejifungua watoto kwa kutumia teknolojia ya IVF, ni jinsi gani watoto wao wanafanya mashuleni, wengi watakuambia kuwa watoto wao ni nadhifu kuliko wa majirani zao! Hii huenda inaonyesha kwamba nikupendwa zaidi kwa watoto hawa.

Mama yetu mkongwe kutoka Uganda alijifungua mtoto mwaka 2009 akiwa na umri wa miaka 62. Mama mkongwe katika ulimwengu wote alijifungua mtoto katika umri wa miaka 67. Yeye alijifungua watoto mapacha wa kike mwaka 1986 huko Romania kupitia teknolojia ya IVF. Bila shaka tunajua katika Biblia mama mkongwe Sarah alipata mtoto akiwa na umri wa miaka 90. Naamini Mungu alikuwa anajaribu kutuambia kuwa tukiamini na kuwa pamoja naye hakuna vikwazo vyovyote. Teknolojia hii ya IVF ni Mungu aliileta.

Kliniki yetu na Hospital ya wanawake na uzazi Uganda, ilikuwa ya kwanza kuwa na mtoto aliyezaliwa kutumia teknolojia ya IVF katika Afriaka Mashariki na Kati.Tunamshukuru Mungu kwa kuwa waanzilishi wa kwanza wa teknolojia hii katika ukanda huu.Tunajivunia kuwa wana Afrika Mashariki.

Tangu wakati huo, watoto zaidi ya 600 wamezaliwa kwa kutungwa mimba kwa njia ya teknolojia ya IVF katika kliniki yetu ya Kampala. Tumeweza kuwasaidia familia nyingi kutoka Tanzania kutimiza ndoto yao ya kuwa na watoto walipotutembelea kliniki yetu ya Kampala na kupata matibabu.

Hawa wanandoa wako tayari kutoa ushuhuda wao. Unaweza pia kuona baadhi ya picha za watoto wao kwenye nyumba yetu ya sanaa kwenye kliniki yetu.
Kliniki yetu ya Dar iko tayari kuongeza kasi na kushirikiana na madaktari wa ndani ya nchi kwa njia ya mafunzo ya semina ambayo itafanyika miezi ijayo kueneza teknolojia hii sehemu mbalimbali za Tanzania.

Si kila kesi ya utasa inahitaji ya teknolojia ya IVF. Kuna njia nyingine za kusaidia uzazi (ART) mbinu kama vile; Kudhibitiwa usisimuaji wa ovari, IUI (Uingizaji wa mbegu kwenye kizazi), Mbegu kuosha kwa wanandoa wenye VVU, ambayo inaweza kutumika katika kuchagua na kusaidia wanandoa tasa katika suala hili.

Mzigo wa Gharama
Teknolojia hii ni ya gharama kubwa katika suala la muda, msongo wa mawazo na hisia, mvutano wa familia kila upande, na suala la fedha.
Tunafahamu haya matatizo na sisi tuko tayari kutoa huduma za ushauri katika kesi ya kila mtu binafsi ili kuhakikisha kwamba wewe unapewa matibabu bora na yanatolewa kwa tatizo/hitaji lako maalumu.

Mwisho, nataka kukuhakikishia kwamba sisi tunatoa asilimia mia moja (100%) ya usiri juu ya mgonjwa na kesi yake. Sisi hatutazidhihirisha kwa mtu yeyote habari yoyote kuhusu matibabu yako hata kama umefanikiwa. Sisi pia tutachukua hatua kali za kinidhamu kwa mfanyakazi wetu yeyote ambaye atajaribu kutoa taarifa yako ya matibabu kwa mwanachama yeyote wa umma. Haya ni kabla ya mahitaji ya maadili matibabu ya kwamba sisi tuna kiwango kikubwa cha utii kwayo.

Huduma zetu

1. Mashauriano
Hii itahusisha kusikilizwa na kupewa ushauri na dakttari katika kliniki yetu. Pia utafanyiwa uchunguzi na dakitari na kama ikibidi utafanyiwa ultrasound ya kizazi. Pia uchunguzi wa ziada kama damu,  uchunguzi wa saratani ya kizazi (pap smear) pale ambapo unahitajika, zitachukuliwa.

2. Ultrasound ya kizazi
Huu ni uchunguzi muhimu sana, ambao unasaidia kuangalia mfuko wa uzazi pamoja na mayai,  na uvimbe wowote ndani ya mfuko wa uzazi na sehemu za karibu yake kwenye matumbo Uchunguzi huu unaweza kufanywa na daktari na taarifa zote zikawekwa kwenye kumbukumbu za mgonjwa.

3. Vipimo vya damu
Vipimo vya kawaida vya damu ni: FSH, E2, Prolactin, LH, TSH na sukari. Homoni za uzazi kawaida zinakadiriwa ndani ya siku tano (5) za kwanza za mzunguko yako wa hedhi. D1 ni siku ya kwanza ya hedhi yako. Kwa wanawake wenye vipindi vya kawaida au wameacha hedhi, kipimo cha homoni za uzazi kinaweza kufanyika bila yakuhusiana na kipindi cha mzunguko wako wa hedhi.

4. X-rays za mirija ya uzazi (HSG)
Hiki ni kipimo muhimu cha uchunguzi. Hata hivyo hakitoi asilimia mia (100%) ya usahihi. Katika baadhi ya matukio inakuwepo haja ya kufanya vipimo vya ziada ili kuhakikisha hali halisi ya mirija yako ya uzazi.

5. Uchunguzi wa kizazi bila upasuaji (Hysteroscopy na Laparoscopy Surgery)
Hii ni njia bora ya kuona na kujua hali halisi ya viungo vya ndani ya tumbo na kizazi. Uchunguzi huu unafanyika kwa siku moja na unaruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyo hiyo, wala sio lazima kulazwa hospitalini kwa siku kadhaa, na dawa ya usingizi huwa inatumika. Ni moja ya uchunguzi muhimu katika kujua usababishaji wa utasa. Daktari anaweza kukufahamisha kwa kina zaidi endapo utahitajika kufanyiwa uchunguzi huu

6. Uchambuzi wa Manii
Huu pia ni uchunguzi muhimu. Sisi tunahitaji kwamba wanandoa wote kuleta vipimo vyovyote vilivyofanyika katika kliniki nyingine. Wakati mwingine tunaweza kurudia baadhi ya vipimo hivyo kwenye kliniki yetu. Mara baada ya kufanya vipimo vilivyotajwa hapo juu, tutakuwa na uwezo wa kufahamu nini zaidi ni tatizo na kisha kupanga matibabu yako.

Mbinu za Kusaidia Uzazi (ART)

a) Usimamamizi wa kusisimua mayai kwa kutumia vidonge na sindano maalum (clomid na FSH)
b) IVF (Upandikizaji)
c) IVF / ICSI (Upandikizaji / Uingizaji wa manii ndani ya uke kwa njia ya sindano) - kwa wanaume wenye kiasi kidogo cha manii
d) Msaada/mchango wa mayai - kwa ajili ya wagonjwa wanawake wenye mayai changa (/ waliomaliza hedhi/ umri mkubwa) / au wenye mayai mabaya
e) Surrogacy (ukodishaji wa mfuko wa uzazi) - Wanawake wasio na mfuko wa uzazi, kwa mfano baada ya kuondolewa mfuko wa uzazi / matatizo ya kutoka kwa mimba mara kwa mara / matatizo ya moyo, figo nk., ambapo mama hawawezi kubeba mimba salama.
f) Uoshaji wa mbegu za kiume kwa wanandoa walioathirika na virusi (mwanaume mwenye VVU) – tuna uwezo wa kusafisha na kutoa virusi vya ukimwi kutoka kwenye mbegu za kiume na kuziingiza kwenye mfuko wa kizazi.
g) Uhifadhi wa embryo, manii, mayai kwa njia ya kitaaluma zaidi
h) PGD (Utambuzi wa Genetic kabla ya upandikizaji) - kwa mfano uchaguzi jinsia ya mtoto (kiume/kike), matatizo ya kiasilia kama kiini mundu / matatizo ya damu kutoganda, nk.

Videos

Sisi pia tunafundisha kwa kutumia videos katika kliniki yetu ambayo utafanyika kwa baadhi ya vipimo ambavyo sisi hufanya ili kumwezesha mgonjwa kuelewa tatizo lake na taswira ya kinachoendelea katika mwili wake.

Taarifa ya matibabu

Kwa kumaliza, utapewa barua fupi/ taarifa fupi ambayo itaelezea jinsi daktari alivyokushauri nini kifanyike kwa sasa au hapo mbeleeni kwa ajili ya matibabu yako Tunaweza pia kutuma waraka huu kwenye barua pepe yako binafsi.

Nini hatufanyi

Hatuwezi kufanya utoaji wa mimba. Sisi ni watu wachamungu (tafadhali angalia imani yetu kwenye tovuti yetu ya Sayansi). Sisi ni kwa ajili ya Uhai na sio kifo. Sisi hapa tuko tayari kukusaidia katika kila njia kuona kwamba unafanikiwa kupata mtoto.

Sanduku la Maoni

Tafadhali weka maoni yako katika sanduku letu la maoni. Hii itatusaidia kutoa huduma nzuri na kuboresha huduma zetu zilizopo kwa sasa na siku za mbele
Nitatumia uwezo na ujuzi wangu nilio nao ili mfanikiwe na kuwa na uwezo wa kufurahia haki na neema ya Mungu ya kuwa na familia.